facebook twitter instagram youtube linkedin tiktok

sabasaba

Awamu ya pili TYC/Sabasaba (2022)

TYC imekuwa ikifanya kazi ya kujenga uwezo na kuongeza uelewa, ambayo mara kwa mara imedhamiria kuwajengea uwezo vijana, na kuwafanya wafahamu nini wanaweza kufanya ili kufikia maendeleo endelevu. Kutokana na dhamira hiyo, TYC imeaandaa Jukwaa maalumu la vijana kushiriki katika maonyesho ya biashara kimataifa SABASABA kwa lengo kuu la kuwapa vijana wajasiriamali nafasi ya kuonyesha na kutangaza biashara zao na shughuli wanazofanya, Kujenga na kukuza mtandao sambamba na kubadilishana uzoefu katika shughuli wanazofanya.

Kutokana na nafasi kuwa chache kwa washiriki kwa mwaka 2021, TYC Imeongeza ukubwa w­­­a banda ili kuwapa fursa vijana wengi zaidi na ambao hawakupata nafasi ya kushiriki Maonyesho.

TYC inapenda kuchukua nafasi hii kutangaza fursa kwa vijana 50 wajasiriamali kushirikia katika Maonyesho yanayo tarajiwa kufanyika mnamo mwezi wa sita mwishoni na wa saba mwanzoni.

Ili kushiriki maonyesho chini ya TYC, mshiriki anapaswa kuchangia kiasi cha pesa taslimu laki mbili na nusu (250,000) ambazo zita jumuisha vitu vifuatavyo kwa muda wote wa maonyesho.

  1. Nafasi
  2. Kiti na Meza moja.
  3. Usafiri wa kubebea meza
  4. Kitambulisho
  5. Cheti cha utambuzi.
  6. Mapambo .

 

Sifa za mshiriki.

  1. Mshiriki anatakiwa kuwa ni Raia wa Tanzania.
  2. Kijana Mwenye umri kati ya miaka 18 na 35.
  3. Awe na biashara.

 

Namna ya kujisajili Ushiriki.

  1. Fanya malipo kupitia namba +255(0)688-271-461.
  2. Tuma ujumbe wa uthibitisho wa malipo kwa baruapepe application@tzyc.org au nambari ya simu
  3. Andika Jina lako kamili ambalo linasoma kwenye nambari ya simu iliyofanya muamala.
  4. Utapokea Stakabadhi ya malipo, kwa baruapepe na nambari ya simu.

Mwisho wa Usajili ni tarehe: 25/05/2022

Hakuna kigezo kuzingatia Jinsia, Dini, Kabila wala Wasifu wa kifedha.  Kama unahitaji Jisajili sasa.