YOUTH ENTREPRENEURSHIP FOR THE FUTURE OF FOOD AND AGRICULTURE
VOICE FOR YOUTH (KILIMO SAUTI PROJECT)
KUHUSU MRADI WA KILIMO SAUTI.
Mradi wa KILIMO SAUTI unalenga kuimarisha uwezo wa vijana katika sekta ya kilimo biashara ili waweze kushiriki kwa ufanisi na kupata faida. Pia, unalenga kuongeza uwezo wao wa kutoa maoni yao na kufanya sera, sheria, na kanuni za kilimo biashara kuwa wezeshi. Mradi huu pia unalenga kuonesha jinsi kilimo biashara kinavyoweza kutoa fursa kwa vijana wakiwemo wenye ulemavu ili
kupata ajira zenye staha.
LENGO LA MRADI WA KILIMO SAUTI.
Uboreshaji wa sera na mazingira ya kisheria ili kuimarisha uwezo wa vijana kwenye ajira zenye staha na zenye kutosheleza
MALENGO MAHSUSI YA MRADI:
- Kuongezeka kwa sauti na ushawishi wa vijana wa kike na kiume katika michakato ya sera na maamuzi.
- Kuongezeka kwa uwezo wa vijana wa kike na kiume katika kutumia fursa za kilimo biashara.
- Kuboresha uelewa, uratibu na ushiriki wa taasisi za vijana katika kilimo biashara.
WASHIRIKA WA MAENDELEO.
Mradi huu unatekelezwa kwa ufadhili wa Mastercard Foundation kupitia AGRA.
WASHIRIKA WENGINE.
Sokoine University Graduate Entrepreneurs’ Cooperative (SUGECO), TanTrade, Vyombo vya Habari, Mitandao ya Vijana, Voice of Youth Tanzania (VOYOTA) na mashirika mengine ya vijana.
MAENEO YANAYOFIKIWA:
Mradi huu utafikia mikoa kumi na tatu (13) Tanzania bara ambayo ni: Kigoma, Kagera, Singida, Katavi Songwe, Mbeya, ringa, jombe Rukwa Dodoma, Manyara, Morogoro, na Ruvuma
WALENGWA WA MOJA KWA MOJA NA WASIO WA MOJA.
Mradi huu unalenga kunufaisha moja Mradi unalenga kufikia matokeo kwa moja vijana 300,000 na kwa njia isiyo ya moja kwa moja Zaidi ya 1,000,000 katika sekta ya kilimo. Kati ya walengwa wa moja kwa moja, mradi utazingatia mgawanyo wa wanuafika kama fuatavyo; 50 % watakuwa vijana wa kike, 30% vijana wa kiume, 5% viongozi wa jamii (wanawake a wanaume), 5% watendaji wa serikali, na 10% watu wenye ulemavu.
SHUGHULI ZINAZOTARAJIWA KUFANYIKA KATIKA MRADI.
Shughuli za mradi zimegawanywa katika makundi yafuatayo:
- Kuwezesha kubadilishana maarifa, kuunganishwa na ushirikiano wa vijana katika mifumo ya chakula na kilimo
- kutumia majukwaa ya kidijitali kufikia na kusambaza taarifa sahihi za kilimo biashara na soko kwa vijana.
- kuongeza uelewa wa vijana na wadau wengine kuhusu fursa za ajira zenye staha zinazotokana na kilimo biashara
- Kuongeza ushiriki wa vijana katika sera na maamuzi kuhusu mazingira wezeshi kwa ushiriki wa vijana katika kilimo biashara.
MATOKEO YANAYOTARAJIWA NA MRADI
Mradi unalenga kufikia matokeo yafuatayo.
- Kuongezeka kwa sauti na ushawishi wa vijana wa kike na kiume katika michakato ya sera na maamuzi
- Kuongezeka kwa uwezo wa vijana wa kike na kiume katika kutumia fursa za kilimo biashara
- kuboresha uelewa,utaratibu,na ushiriki wa taasisi za vijana katika kilimo biashara
NAFASI YA SERIKALI KATIKA MRADI.
- Kuandaa mazingira wezeshi kwa ushiriki vijana katika kilimo biashara
- kuunda mazingira mazuri ya utekelezaji wa shunguli za mradi
- kutoa huduma, ruzuku, taarifa za hali ya hewa , na fursa za upatikanaji wa huduma za serikali kwa wakulima vijana kupitia serikali za mitaa, maafisa ugani,na mamlaka ya haliya hewa Tanzania ( TMA)











