TANGAZO LA MUALIKO KWA VIJANA โ€“ MAONESHO YA SABASABA 2025

Je, wewe ni kijana mbunifu, mjasiriamali au una mradi wenye tija kwa jamii?
Fursa imefunguka kwa vijana kushiriki kwenye Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yatakayofanyika kuanzia Juni 28 hadi Julai 13, 2025, katika viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba Grounds), Barabara ya Kilwa โ€“ Dar es Salaam.

Lengo la Ushiriki

Kuwajengea vijana uwezo wa kibiashara, kuwasaidia kupata masoko ya bidhaa/huduma zao, kukuza mitandao ya biashara, pamoja na kuwatambulisha kitaifa na kimataifa.

Vigezo vya Ushiriki

  1. Umri kati ya miaka 18 hadi 35
  2. Awe Mtanzania
  3. Awe anajishughulisha na biashara, ubunifu, kilimo, sanaa, au mradi wa kijamii
  4. Awe na bidhaa/huduma inayokidhi viwango na mahitaji ya soko
  5. Awe na uthibitisho wa shughuli anayofanya (picha, leseni, TIN, n.k.)
  6. Awe tayari kushiriki maonesho kwa kipindi chote
  7. Atachangia Shilingi 250,000 kwa ushiriki, ambapo:
    • 200,000 ni kwa ajili ya nafasi ya kuonesha bidhaa, kitambulisho, cheti cha ushiriki, matangazo, mafunzo ya biashara, na fursa za masoko
    • 50,000 ni kwa ajili ya gharama za uendeshaji na huduma za msingi

Faida za Ushiriki

1.Utapata cheti cha ushiriki kutoka SIDO

2.utapata semina mbalimbali za ujasiriamali zitakazo tolewa na SIDO,BRELA na nk

3.Utapata huduma za usaili wa biashara kama TIN number,Account za benki na nk

4.Nafasi ya kuonesha bidhaa/huduma zako kwa maelfu ya watu

5.Utapa kitambulisho na ulinzi w bidhaa wakati wote wa maonesho

6.Kutangaza biashara yako kupitia majukwaa ya ndani na nje

7.Kujifunza mbinu bora za biashara na masoko

8.Kupanua mtandao wa wateja na wabia wa biashara

Jinsi ya Kutuma Maombi

Pakua fomu ya ushiriki kupitia https://forms.gle/98jwDLD9QbZXTy4JA au wasiliana nasi kwa:
๐Ÿ“ž [Namba ya simu] | โœ‰๏ธ [Barua pepe] | ๐Ÿ“ [Anuani ya ofisi]
Mwisho wa kutuma maombi: Mei 31, 2025